Wakenya katika miji na vituo vya mijini wameonywa dhidi ya kutupa taka katika mifumo ya mitaro ya maji, mito na mabomba ya maji ya mvua kabla ya mvua inayotarajiwa ya El Niño kati ya Oktoba na Disemba. Mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Operesheni za majanga David Samoei alisema serikali za kitaifa na za kaunti zinafungua njia za maji ili kujiandaa kwa mvua kubwa. Alionya kwamba utupaji taka kiholela unazuia juhudi za kuzuia na kupunguza mafuriko.


DAVID SAMOEI – DUMPING