Wakaazi na viongozi katika Kaunti ya Pokot Magharibi wameunga mkono shughuli zinazoendelea za usalama za mashirika mengi ili kupunguza ujambazi na kurejesha amani. Wakiongozwa na waziri wa zamani Samuel Poghisio, viongozi hao walitaka mabadiliko ya mawazo kupitia elimu na mafundisho ya kidini ili kukuza amani na maendeleo katika eneo hilo. Pia walihimiza serikali kuimarisha shughuli za usalama huku shule zikifunguliwa tena kwa muhula wa tatu, kuhakikisha mazingira salama kwa wanafunzi na wakaazi.

VOX POP-SECURITY