Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amewasihi viongozi wa kisiasa kuheshimu haki ya kidemokrasia ya Wakenya ya kuchagua viongozi wanaowapendelea kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Akizungumza mjini Kitale, Uhuru alitaka kampeni za amani na uvumilivu wa kisiasa. Pia alilaani juhudi za kuwazuia wanasiasa wapinzani kufanya mikutano katika maeneo yanayochukuliwa kuwa ngome za vyama au viongozi fulani.

UHURU KENYATTA-RIGHT