Baada ya miezi mitano nje ya uwanja kufuatia jeraha la paja lililohitaji upasuaji mwezi Aprili, nahodha wa Harambee Stars, Michael Olunga, alirejea uwanjani Ijumaa. Olunga alitoka benchi kwa Al Arabi katika pambano la ligi ya Qatar dhidi ya Al-Shamal, ambalo lilimalizika kwa sare ya 2-2. Kurudi kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ni nyongeza kubwa kwa Harambee Stars wanapojiandaa kwa mechi zao muhimu za kufuzu AFCON za Septemba 2027 dhidi ya Eritrea, Guinea na Afrika Kusini katika kundi D.

 

Yomif Kejelcha wa Ethiopia alirejesha rekodi ya dunia ya nusu marathon baada ya kukimbia kwa muda wa dakika 56 sekunde 51 katika Marathon ya Buenos Aires huko Argentina jana. Kejelka alipunguza sekunde 29 kutoka kwa rekodi ya awali ya nusu marathon ya dakika 57 sekunde 20, iliyowekwa na Jacob Kiplimo wa Uganda huko Lisbon. Aliwashinda wenzake Tadese Worku na Bereket Nega kwa mpangilio huo. Katika mbio za wanawake, Fotyen Tesfay wa Ethiopia aliibuka mshindi kwa dakika 1 sekunde 3. Wakimbiaji waliozaliwa Kenya waliogeuka kuwa raia wa Uturuki, Nevin Can na Selin Can walimaliza wa pili na wa tatu mtawalia.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kericho, Kisumu na Eldoret.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.