Serikali inawasihi wale wote ambao wameshambuliwa na wahuni wakati wa mikutano ya kisiasa kurekodi taarifa kwa mamlaka ili hatua zinazofaa zichukuliwe. Waziri wa Usalama  Kipchumba Murkomen anasema serikali iko njiani kukomesha utamaduni wa uhuni nchini. Alipuuza madai kwamba hali ya usalama ni mbaya, akisema viongozi wa upinzani wanazidisha hali hiyo. 

KIPCHUMBA MURKOMEN –REPORT