Ni afueni kubwa kwa wakulima kabla ya msimu ujao wa kupanda kufuatia hatua ya serikali ya kupunguza gharama ya pembejeo muhimu za shambani. Rais William Ruto anasema bei ya mbegu za mahindi itapunguzwa kwa asilimia 50 kuanzia mwezi ujao, kutoka shilingi 300 hadi 150 kwa kila mfuko. Bei ya mbolea pia itashuka kwa shilingi 500, kutoka shilingi 2,500 hadi 2,000 kwa kila gunia, ili kuwahimiza wakulima kupanda mahindi zaidi wakati wa mvua fupi.

WILLIAM RUTO-REDUCE