Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen ametoa wito kwa upinzani kushirikiana na serikali katika kukomesha utamaduni wa uhuni nchini. Akizungumza huko Trans Nzoia jana, Murkomen aliwashutumu baadhi ya viongozi wa upinzani kwa kudhoofisha vita hivyo kwa kutoa wito wa kuachiliwa huru kwa washukiwa waliokamatwa kwa kosa hilo. Alisisitiza kwamba hali ya usalama nchini Kenya bado inadhibitiwa na kuwashutumu baadhi ya viongozi kwa kuzidisha hali hiyo ili kusababisha wasiwasi usio wa lazima.
KIPCHUMBA MURKOMEN –SECURITY