Naibu Rais Kithure Kindiki ametoa wito kwa serikali za kaunti kujiandaa vya kutosha kwa ajili ya mvua inayotarajiwa ya El Nino. Akizungumza wakati wa kikao cha 30 cha kawaida cha IBEC katika makaazi yake Karen, Kindiki alisema serikali ya kitaifa imeongeza maandalizi ikiwa ni pamoja na kuweka vifaa vya misaada katika maeneo yaliyo na hatari na kuziba mifumo ya mifereji ya maji ili kuzuia na kupunguza matukio ya mafuriko.


KITHURE KINDIKI – PREPOSITION