Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua leo atakutana na wajumbe kutoka Isiolo na Marsabit, pamoja na wawakilishi wa Gen Z, wakikamilisha wiki kadhaa za mazungumzo mazito ya kijamii katika makaazi yake ya Wamunyoro. Baada ya hapo, Gachagua atafanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea mwelekeo wake wa kisiasa kabla ya kuanza ziara ya Marekani ya kuzungumza na Wakenya wanaoishi ughaibuni na washirika wa Marekani Jumatano.