Waziri wa Elimu Julius Ogamba amekosoa baadhi ya wanasiasa kuhusu kile alichokielezea kama kuendelea kwa siasa za Kenya kuwa za kikabila, akisema matamshi hayo sasa yanawaathiri wanafunzi. Ogamba alisema vijana wa Kenya hawapaswi kufundishwa kuangaliana kupitia macho ya utambulisho wa kikabila, akisema kwamba jumbe za kisiasa zinazohimiza jamii kuwaweka wengine mbali haziendani na hali halisi ya jamii ya Kenya.

JULIUS OGAMBA - HATE