Michuano ya US Open itatoa hazina kubwa zaidi ya zawadi katika historia ya Grand Slam ikiwa na jumla ya dola milioni 108, ambayo ni ongezeko la 20% ikilinganishwa na mwaka uliopita. Mabingwa wa singles watapata dola milioni 5.5 kila mmoja katika ongezeko la 10% kufikia mwaka 2025. Washindi wa raundi ya kwanza watachukua dola milioni 140 na 27% zaidi ya mwaka uliopita. Zawadi hiyo inajumuisha mchango wa dola milioni 2 kwa hazina ya ustawi, ambayo wachezaji wakuu wamekuwa wakiitisha kutoka kwa Grand Slam zote.

 

Mabingwa wa KPL Gor Mahia watapambana na washindi wa kombe la FKF Tusker katika Kombe la FKF Super Cup Jumapili, huku pande zote mbili zikitarajia kuanza msimu mpya na medali. KO’gallo ambao wamemaliza wa pili katika mashindano ya CECAFA nchini Rwanda hawana majeraha mapya na wanatarajia kuwashinda wapinzani wao hadi mechi ya ufunguzi wa msimu. Wakati huo huo, Tusker waliobanduliwa katika hatua ya makundi ya CECAFA watataka kujikomboa huku kocha mkuu Leon Mette akizindua wachezaji wake wapya. Mechi hiyo itaanza saa tisa adhuhuri.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Kajiado na Narok.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.