Lionel Messi alifunga bao lake la kwanza tangu kifo cha baba yake mapema mwezi huu katika sare ya 2-2 kati ya Inter Miami na Philadelphia Union. Messi alifunga bao la pili dakika ya 26, baada ya Daniel Pinta kufuta bao la kwanza la Indiana Vasselie dakika ya 11 na kuwapa Miami uongozi wa 2-1 katika kipindi cha kwanza. Hata hivyo, Cavan Sullivan alisawazisha dakika ya 92 na kulazimisha sare. Matokeo hayo yaliifanya Miami iendelee kuwa ya pili kwenye jedwali la Eastern Conference kwa pointi saba nyuma ya Nashville ambayo iliwashinda New York Redbulls 1-0.

 

Barcelona wamemaliza harakati zao za kumtafuta mshambuliaji Julián Álvarez na wanachunguza chaguzi zingine kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa. Hata hivyo, Barça hawajakataa kurudi kwa Álvarez wakati fulani labda Januari. Kusita kwa Atlético Madrid kumhamisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina kumemlazimisha mkurugenzi wa michezo Deco kutathmini njia mbadala huku Lautaro Martínez wa Inter Milan akiwa juu ya orodha. Kocha wa Barça, Hansi Flick, anasisitiza kusajiliwa kwa mchezaji nambari 9 ili kufidia kuondoka kwa Robert Lewandowski na Ferran Torres.

Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.