Seneta wa Nyandarua John Methu anasema eneo la Mlima Kenya halitagawanyika kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Akizungumza huko Kiharu, Methu alidai kuna mipango ya kugawanya eneo hilo kisiasa, lakini akasema wakaazi watapinga majaribio yoyote ya kugawanya kura zao. Alisema eneo hilo litapiga kura kama kundi moja, kama lilivyofanya katika chaguzi zilizopita, na kupinga kile alichokiita juhudi zinazofadhiliwa na serikali za kuunda vyama kadhaa vya siasa mlimani.

JOHN METHU - MT KENYA