Kiongozi wa Chama People's Party, Ndindi Nyoro, anasema chama hicho kinapata wafuasi na umaarufu, akisisitiza kuwa si kibaraka wa serikali. Akizungumza baada ya kuwakaribisha wajumbe 30 kutoka vyama mbalimbali katika makao makuu yake jijini Nairobi, Mbunge huyo wa Kiharu aliendelea kukosoa utawala wa Rais William Ruto na polisi kuhusu kuongezeka kwa matukio ya uhuni kote nchini. Alikaribisha wito wa Upinzani wa ulioungana wa kutaka ICC ichunguze uovu huo na kuchukua hatua dhidi ya wahusika.


NDINDI NYORO - REMARKS