Wapelelezi wanachunguza kifo cha mfanyakazi wa nyumbani mwenye umri wa miaka 36 ambaye alipatikana amefariki katika nyumba moja huko Kilimani, Nairobi, katika tukio linaloshukiwa kuwa kujitoa uhai mapema Jumatano asubuhi. Mwanamke huyo, aliyetambuliwa kama Grace Akinyi, alipatikana akining'inia kwenye grill ya ngazi yapata saa kumi na mbili asubuhi. Polisi walisema tukio hilo liliripotiwa na mlinzi, ambaye aliwaambia maafisa kwamba aliamka na kuwakuta wapangaji wamekusanyika kwenye ngazi.