Marehemu Gloria Khalwale, mke wa Seneta wa Kakamega Boni Khalwale, anatarajiwa kuzikwa hii leo huko Malinya katika Kaunti Ndogo ya Ikolomani, Kakamega. Mazishi hayo yanatarajiwa kuvutia viongozi wa kisiasa kutoka kambi za serikali na upinzani. Gloria alifariki Jumamosi iliyopita baada ya kupata mshtuko wa moyo.