Naibu Rais Kithure Kindiki amemkosoa kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua kwa madai ya kudhoofisha uongozi wa Mlima Kenya Mashariki na kuwachochea wakaazi kukataa serikali. Akizungumza huko Tharaka Nithi, Kindiki alisema si haki kukuza uadui dhidi ya serikali kwa sababu tu sehemu moja ya eneo hilo haina nyadhifa muhimu za serikali. Aliahidi kukuza ajenda ya maendeleo ya serikali katika eneo hilo lote na kuhakikisha sehemu zote za Mlima Kenya zinahusika katika programu za serikali.


KITHURE KINDIKI-UNFAIR