Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe anasema Kenya inapanga kuwekeza katika miundombinu ili kuongeza uvunaji wa maji na kusaidia kilimo cha kiwango kikubwa. Alisema uvunaji wa maji ya mito, kujenga na kurekebisha mabwawa, na kuchimba visima zaidi kutaongeza uzalishaji wa chakula na kupunguza utegemezi wa mvua isiyoaminika. Kagwe alisema Kenya haiwezi kuruhusu kiasi kikubwa cha maji ya mvua kupotea wakati wa misimu ya mvua huku jamii baadaye zikikabiliwa na uhaba wa maji na ukosefu wa usalama wa chakula.

MUTAHI KAGWE - UKAME