Kaunti ya Jiji la Nairobi imetoa notisi ya siku saba kwa umma kutambua na kuichukua miili 59 ambayo haijadaiwa iliyo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Mama Lucy Kibaki. Katika notisi ya umma kaunti hiyo ilisema miili hiyo imesalia katika kituo hicho kuanzia tarehe ilipoletwa huku ikisubiri kuchukuliwa. Kaunti inawaomba jamaa, marafiki na umma kuangalia orodha hiyo na kutambua miili yoyote.