Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru ametoa wito wa kukomeshwa kwa vurugu za aina zote, akiwahimiza Wakenya kulinda nafasi ya kidemokrasia ya nchi. Waiguru anasema wale waliopewa jukumu la kudumisha amani na usalama lazima watekeleze majukumu yao bila upendeleo na kwa ufanisi, akisisitiza kwamba Kenya ni nyumba ya pamoja ambayo lazima ilindwe kwa vizazi vya sasa na vijavyo.