Katibu wa Cotu Francis Atwoli amepata ushindi wa kisheria baada ya Mahakama ya leba kufuta ombi lililopinga kuchaguliwa kwake tena kama Katibu Mkuu wa COTU. Jaji Jemimah Keli, akitoa uamuzi huo jana, aliamua kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kuamua ombi lililowasilishwa na Fazul Mahamed na Taasisi ya Utawala wa Kidemokrasia. Walalamikaji walikuwa wamepinga uchaguzi huo, ambapo Atwoli alipata muhula wa sita kama Katibu Mkuu, wakisema ulifanywa kabla ya vyama washirika kukamilisha michakato yao ya uchaguzi.