Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua anasema chama hicho kitafanya uteuzi huru na wa haki katika Kaunti ya Laikipia, bila mgombea yeyote kupata upendeleo. Akizungumza baada ya kukutana na wagombea wanaotarajiwa, Gachagua aliwahakikishia kwamba wagombea wote watakuwa na fursa sawa ya kushindana. Anasema chama hicho hakitawalazimisha wagombea, huku kikijitayarisha kuimarisha miundo yake na kuwasilisha wagombea kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027.
RIGATHI GACHAGUA - NOMINATIONS