Akina mama tisa kati ya kumi sasa wanajifungulia katika vituo vya afya, hali inayochangia kupungua kwa vifo vya akina mama kote nchini. Mkurugenzi Mkuu wa Afya Patrick Amoth anasema huduma za uzazi ziko kikamilifu chini ya SHA. Akizungumza wakati wa mkutano wa afya unaoendelea, Amoth aliongeza kuwa Wizara ya Afya iko katika njia ya kuongeza ufadhili kupitia hazina ya Afya ya Msingi ili kuimarisha ubora wa huduma ya kinamama katika vituo vya afya.

PATRICK AMOTH-MORTALITY