Viongozi kutoka nje ya eneo la Mlima Kenya wanaounga mkono serikali, wanakosoa msukumo unaoongezeka wa kuunda vyama kadhaa vya kisiasa katika eneo hilo. Wakiongozwa na Mbunge wa Mugirango Kusini Silvanus Osoro, viongozi hao wanasema hatua hiyo inaweza kusababisha mgawanyiko miongoni mwa viongozi wa Mlima Kenya na kudhoofisha umoja wao wa kisiasa. Wanasema kwamba ushindani wa ndani miongoni mwa kile wanachokielezea kama vyama vya kikabila unaweza kuisadia azma ya Rais William Ruto ya kuchaguliwa tena.
SILVANUS OSORO -