Venus Williams amepewa Wildcard ya kucheza US Open singles, huku dadake mdogo Serena akitarajiwa kujiunga naye huku nafasi moja ikiwa imesalia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 46, alicheza kwa mara ya kwanza New York, miaka 29 iliyopita na akafika fainali katika mechi yake ya kwanza ya singles mwaka wa 1997. Mmarekani huyo alishinda mataji mawili kati ya saba ya Grand Slam singles katika uwanja wa Flushing Meadows mwaka wa 2000 na 2001. Venus na bingwa wa mwaka 2017 Sloane Stephens wanaungana na Carol Young, Reese Brantmeier na Thea Frodin.
Kiungo wa kati wa Bayern Munich, Jamal Musiala, amefichua kwamba anakabiliwa na kifafa kinachoweza kutibika baada ya kuanguka uwanjani kwa mara ya pili ndani ya siku nne. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23 alianguka muda mfupi baada ya kuingia katika mechi ya kirafiki ya Jumanne huko Heidenheim kama mchezaji mbadala katika kipindi cha pili. Wachezaji kutoka timu zote mbili walimzunguka Musiala alipokuwa akipatiwa matibabu. Kisha alisaidiwa alipotoka uwanjani. Musiala alikuwa ameanguka Jumamosi wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya RB Leipzig.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.