Rais William Ruto anasema lengo la serikali sasa ni kuifanya UHC ifanye kazi vizuri zaidi kwa kila mgonjwa, kituo cha afya na kaunti. Rais anasema maeneo ya kipaumbele ni pamoja na kurahisisha usajili, kuelezea wazi faida zinazopatikana kwa wanachama, kuharakisha malipo ya madai na kufanya mifumo ya afya ya kidijitali kuwa rahisi zaidi. Anasema maboresho hayo ni muhimu ili kuhakikisha Wakenya wanapata huduma bora na zenye ufanisi zaidi za afya chini ya mageuzi yanayoendelea.
WILLIAM RUTO - TASK