Wataalamu wa matibabu wanatoa wito wa kuimarishwa kwa uchunguzi wa watoto wachanga na utambuzi wa mapema wa ugonjwa wa Sickle Cell ndani ya wiki sita za kwanza za maisha ili kupunguza matatizo. Akizungumza wakati wa Mkutano wa Afya wa Kenya unaoendelea, daktari Brenda Misori alisema utambuzi wa kuchelewa umesababisha wagonjwa wengi kutafuta huduma baada ya kupata kiharusi na maumivu ya mara kwa mara. Kenya inarekodi takriban visa elfu 14 vya sickle cell, huku mzigo mkubwa zaidi ukiripotiwa katika kaunti 17 kote Magharibi mwa Kenya na Nyanza.

BRENDA MISORI-SICKLE