Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua na Gavana wa Busia Paul Otuoma wameitwa na tume ya Uiano NCIC kutokana na matamshi yao wakati wa mikutano ya hadhara. Gachagua anatarajiwa kufika mbele ya tume hiyo Alhamisi wiki ijayo huku Gavana Otuoma akipangwa kufika mbele ya tume hiyo Ijumaa hii. Tume hiyo inasema matamshi yao yanaweza kutishia umoja wa nchi.