Wanawake wanaowania uongozi wa kisiasa wamehimizwa kubaki makini licha ya kukatishwa tamaa na wakosoaji. Kiongozi wa chama cha PLP Martha Karua anasema wanawake lazima wajenge imani kubwa na kukataa kuzuiwa na wanaopinga. Karua anawataka wanawake kutumia kila kitu walichofanya kwa ajili ya jamii zao na kukitumia kama msingi wa kutafuta viti vya kuchaguliwa. Anasema wanawake lazima waamini wanaweza kufanikiwa katika siasa.
MARTHA KARUA - IGNORE