Viongozi kote nchini wanaendelea kulaani vurugu zilizoshuhudiwa huko Homa Bay Jumapili iliyopita, ambazo zilisababisha afisa mmoja wa polisi kufariki na raia kadhaa kujeruhiwa. Mbunge wa Samburu Magharibi, Naisula Lessuda, amejiunga na wale wanaolaani vurugu na vitisho, akisema tofauti za kisiasa hazipaswi kamwe kuhalalisha mashambulizi dhidi ya Wakenya, waandishi wa habari, viongozi au uharibifu wa mali.
NAISULA LESSUDA – VIOLENCE