Baraza la Wazee la Kirinyaga limemkosoa Naibu Rais Kithure Kindiki kwa matamshi wanayosema yanalenga kugawanya kaunti kwa misingi ya kikanda. Wazee hao wakiongozwa na John Gathungu walipinga madai kwamba maeneo bunge ya Mwea na Gichugu ni ya Mlima Kenya Mashariki, huku sehemu iliyobaki ya Kirinyaga ikiwa chini ya Mlima Kenya Magharibi. Walisisitiza kwamba Kirinyaga ni kaunti moja na haipaswi kugawanywa kwa misingi ya kisiasa au kikanda, wakisisitiza kwamba kaunti hiyo ina uongozi mmoja chini ya Gavana Anne Waiguru.
JOHN GATHUNGU – KINDIKI