Morocco ndiyo taifa linaloongoza barani Afrika lenye idadi kubwa zaidi ya viwanja vilivyoidhinishwa na CAF, ikiwa na viwanja 16 vilivyoidhinishwa kwa sasa. Afrika Kusini inafuata ikiwa na viwanja 13, huku Misri ikishika nafasi ya tatu ikiwa na viwanja 8. Algeria inajivunia viwanja 7 ikifuatiwa na Mali na Cameroon ikiwa na viwanja 5 kila kimoja, huku Libya, Tunisia, Uganda na Angola zikiwa na viwanja vitatu kila kimoja. Waandaaji wenza wa AFCON mwaka 2027 Kenya, na Tanzania ina viwanja viwili kila kimoja, huku Zanzibar, Sudan Kusini na Gambia zote zikiwa na kimoja. Benin, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Djibouti, Eritrea Somalia na Sudan hazina viwanja vilivyoidhinishwa.


 Mabingwa wa kitaifa wa msururu wa Raga ya Sevens ya Sportpesa KCB, wameelekeza mawazo yao kwa Driftwood 7s, huku wakitafuta ushindi wao wa tatu msimu huu. Kocha mkuu wa wanabenki, Andrew Amonde, anaamini wana kila linalohitajika kushinda Mombasa licha ya ushindani mkali na halijoto ya juu. Baada ya kushinda misururu miwili kati ya mitatu, wanabenki wataendelea na ulinzi wao wa taji dhidi ya Blak Blad, Kisumu RFC na Emerging 7s katika Kundi B. Huyu hapa Amonde.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Kajiado na Narok.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.