Mbunge wa Homa Bay Mjini, Peter Kaluma, ameitwa na tume ya uiano NCIC kutokana na matamshi yake kabla ya mkutano wa Linda Mwananchi uliofanyika Jumapili iliyopita huko Homa Bay ambao ulikumbwa na vurugu. Kulingana na NCIC, matamshi ya Kaluma aliyotoa kwa lugha yake ya asili kwa mkutano aliokuwa akihutubia yalikuwa na uwezekano wa kusababisha mvutano.