Idara ya utabiri wa Hali ya Hewa nchin inatabiri hali ya ukavu katika sehemu nyingi za nchi katika siku saba zijazo. Hata hivyo, mvua inatarajiwa katika sehemu za kaunti za Bungoma, Trans Nzoia, Nakuru, Uasin Gishu, Kisii, Lamu, Kericho, Nyandarua na Nyeri. Pia inatabiri hali ya baridi na mawingu ya mara kwa mara katika sehemu za Embu, Kiambu, Kirinyaga, Laikipia, Meru, Murang'a, Nairobi, Tharaka-Nithi, Machakos, Kajiado na Marsabit.