Gavana wa Siaya James Orengo ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja kufuatia machafuko yaliyovuruga mkutano wa hadhara wa Linda Mwananchi huko Homa Bay jana. Orengo aliwashutumu polisi kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya wahuni na viongozi wa kisiasa anaodai kuwa waliwachochea wakaazi kabla ya mkutano huo. Anasema mwitikio wa polisi unaibua maswali mazito kuhusu ulinzi wa haki ya raia ya kukusanyika kwa amani.



JAMES ORENGO – POLICE