Wanaharakati nchini Kenya wameapa kufanya maandamano kesho wakitaka majibu kuhusu kutekwa nyara na kuhamishwa kwa mwanasiasa wa upinzani wa Uganda Kizza Besigye. Wakizungumza na waandishi wa habari, wanaharakati hao waliishutumu Kenya kwa kuhusika katika kuzuiliwa kwa Besigye baada ya kukamatwa nchini humu mnamo Novemba 2024 na kupelekwa Uganda. Pia waliibua wasiwasi kuhusu madai ya vitisho dhidi ya Besigye na mkuu wa jeshi la Uganda na mwana wa Rais Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba.

HUSSEIN KHALID - SUPRESSION