Gavana wa Siaya James Orengo amelaani uhuni wakati wa mkutano wa Linda Mwananchi huko Homa Bay. Orengo anasema majaribio ya kuzuia mkutano huo, ikiwa ni pamoja na kuweka vizuizi barabarani, yanadhoofisha haki ya kujieleza kisiasa kwa amani. Anasema uhuru wa kuishi pamoja licha ya tofauti za kisiasa ni kanuni iliyopigiwa debe kwa miaka mingi na marehemu Raila Odinga, ambaye waandaaji wa mkutano huo wanamtii. Gavana Orengo ametoa wito wa uvumilivu na heshima kwa mitazamo tofauti ya kisiasa.
JAMES ORENGO – CONDEMN