Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amedai kwamba vurugu zilizoshuhudiwa Homa Bay ni sehemu ya njama iliyopangwa ya kuahirisha Uchaguzi Mkuu wa 2027. Akizungumza huko Kithimani, Kaunti ya Machakos, Kalonzo alitoa wito wa kujiuzulu kwa Katibu wa usalama Raymond Omollo kutokana na machafuko hayo. Alionya kwamba matumizi ya wahuni katika siasa hayatavumiliwa, akiwahimiza viongozi kudumisha amani na michakato ya kidemokrasia.
KALONZO MUSYOKA - CHAOS
Read Also