Maeneo mengi nchini yanatarajiwa kusalia na ukavu kwa ujumla katika wiki moja ijayo, huku mvua ikitabiriwa katika kaunti nane, kulingana na idara ya Hali ya Hewa nchini. Utabiri unaonyesha kwamba Bungoma, Trans Nzoia, Nakuru, Uasin Gishu, Elgeyo Marakwet, Kericho, Nyandarua na Nyeri zinaweza kupata mvua katika kipindi hicho.