Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja amewaonya makamanda wakuu wa polisi kuimarisha usimamizi na uwajibikaji, akisema maafisa wanaohusika katika uhalifu hawataruhusiwa kuharibu sifa ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi. Kanja alisema mwenendo wa uhalifu unaofanywa na maafisa unasaliti kiapo chao cha kuwatumikia na kuwalinda Wakenya. Pia aliwaonya makamanda wanaoruhusu magenge na makundi ya wahalifu kufanya kazi kwa uhuru katika maeneo yao.
DOUGLAS KANJA - GOONISM