Licha ya uamuzi wa Mahakama ya Migogoro ya Michezo kuunga mkono Kanuni za FKF za 2025 na FKF baadaye kutoa ratba ya mechi za KPL za mwaka 2026/27 jana, ligi bado inaweza isianze kama ilivyopangwa tarehe 29 mwezi huu. Kutokuwa na uhakika huko kunafuatia amri ya kihafidhina iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Murang'a, ikizuia FKF kutekeleza kanuni za 2025 au kuanza msimu mpya ikisubiri uamuzi wa kesi inayopinga uhalali wake. Mahakama pia imepangwa kusikiliza ombi la kudharau mahakama dhidi ya Rais wa FKF Hussein Mohammed.
Timu ya Raga ya Kenya ya wachezaji wa chini ya miaka 20 Chipu iliishinda Namibia 33-14 na kushinda kombe la Barthez kwa mara ya nne katika uwanja wa Mutesa 2 jijini Kampala Uganda jana. Tries za Michael Lukusi na Jackson Siketi zilishuhudia Kenya ikiongoza kwa 14-0 wakati wa mapumziko, kabla ya Lukusi kukamilisha touch downs zake mbili mawili zikifuatiwa na za Rayvon Ambale na Randy Otuoma. Ushindi huo uliifanya Kenya kurudi kileleni mwa raga ya umri ya Afrika chini ya muundo mpya wa Kitengo cha Utendaji, baada ya kukabidhi taji kwa Namibia mnamo mnamo 2025.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.