Rais William Ruto ataongoza kitengo cha serikali kuu katika kuwasilisha mapendekezo ya mpango wa mageuzi ya kiuchumi wa ruwaza ya mwaka 2060 wakati wa mazungumzo ya kitaifa  asubuhi ya leo katika KICC. Majadiliano hayo yanatarajiwa kufafanua ajenda ya nchi baada ya ruwza ya mwaka 2030, ikizingatia taasisi imara, rasilimali watu, na maendeleo jumuishi. Mazungumzo hayo yanatarajiwa kutoa jukwaa la kuchunguza vipaumbele vya muda mrefu vya Kenya na kuimarisha misingi ya sera muhimu ili kuanzisha na kudumisha maendeleo ya kiuchumi.