Serikali ya Kaunti ya Kitui imekiri kukabiliwa na changamoto ya kulipa Sh milioni 155 zilizotolewa kama mikopo isiyo na riba kwa vikundi mbalimbali wakati wa uchaguzi wa 2022. Alipokuwa mbele ya Kamati ya Seneti ya Uwekezaji wa Umma, Gavana wa Kitui Julius Malombe aliwafahamisha maseneta kwamba mikopo iliyotolewa wakati wa utawala wa gavana Charity Ngilu haikuwa na bima kama inavyotakiwa kisheria. Kati ya Sh milioni 160 zilizotolewa kwa vikundi hivyo, Sh milioni 5 pekee ndizo zilizolipwa.
JULIUS MALOMBE - TEAMS