Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeanza maandalizi mapya ya Uchaguzi Mkuu wa 2027, ikialika zabuni za usambazaji na matengenezo ya teknolojia na vifaa muhimu vya uchaguzi. Kupitia notisi ya zabuni tume hiyo iliwaalika wazabuni wanaostahiki kutoa, kusakinisha, kujaribu, kuagiza na kudumisha Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Uchaguzi wa Kenya (KIEMS), ikiwa ni pamoja na vifaa, vinavyohitajika.