Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Renson Ingonga anasema ofisi yake iko tayari kushughulikia makosa ya uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Ingonga anasema kitengo maalum chenye waendesha mashtaka waliofunzwa maalum kimeanzishwa kushughulikia uhalifu wa uchaguzi. Anaonya kwamba wale wanaohusika katika vurugu, hotuba za chuki, uhalifu wa mtandaoni na vitisho watakabiliwa na sheria. Ingonga anasema ODPP itafanya kazi na mashirika ya uchunguzi ili kuhakikisha uchaguzi wa amani.

RENSON INGONGA – REPORTING