Wazazi humu nchini wamehimizwa kuwaonya watoto wao dhidi ya kujihusisha na kamari, hasa shughuli haramu za kamari zinazokiuka sheria za nchi. Naibu Kamishna wa Kaunti ya Malindi Harrison Mwatevwa alisema baadhi ya shughuli zinazofanyika katika eneo hilo zinachangia pakubwa katika kuporomoka kwa maadili ya vijana. Alibaini kuwa kamari inaweza kuathiri vibaya tabia ya mtoto, utendaji wake kitaaluma, na ustawi wake kwa ujumla, na akawataka wazazi kuchukua jukumu la kuwaongoza na kuwafuatilia watoto wao.

HARISSON MWATEVWA – GAMBLING