Mgombea urais wa Chama cha United Green Movement, David Maraga, anatarajiwa kuhitimisha ziara yake ya kampeni ya siku tatu katika Kaunti ya Taita Taveta leo. Maraga, ambaye alianza ziara hiyo Alhamisi alifanya mikutano na wazee, vijana na wataalamu huko Voi kabla ya kuelekea Mwatate kwa mazungumzo na viongozi wa mashinani na wajumbe. Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi zake za kutangaza azma yake ya urais kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027.

DAVID MARAGA – TAITA TAVETA