Harakati ya Linda Mwananchi imekanusha madai kwamba Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna hana uzoefu wa kugombea urais, ikisema uongozi wa sasa chini ya Rais William Ruto umeshindwa. Harakati hiyo pia iliishutumu serikali kwa kuhamasisha makundi kwenda Ikulu ili kuunga mkono azma ya rais kuchaguliwa tena. Wakizungumza katika mkutano huko Busia, viongozi hao waliwasihi wakaazi kuungana nyuma ya Sifuna wakimtaja kama nafasi kubwa zaidi ya jamii ya Waluhya ya kumtoa rais ajaye wa Kenya.
EDWIN SIFUNA - EXPERIENCE