Chama cha Safina cha Jimi Wanjigi kimekaribisha uamuzi wa Mahakama Kuu uliotangaza kwamba Uchaguzi Mkuu ujao wa nchi unapaswa kufanyika mwezi huu na sio Agosti mwaka ujao. Kulingana na chama hicho, uamuzi huo uliunga mkono uhalali wa kikatiba na kuitaka nchi kuheshimu. Katika hukumu ya kihistoria, Jaji Mugure Thande alisisistiza kwamba mwaka wa tano kufuatia Agosti 9, 2022, uchaguzi wa rais ulifaa kufanywa Agosti 9, 2026, ikimaanisha uchaguzi ujao wa rais unapaswa kufanyika ndani ya mwaka huo wa tano kama inavyotakiwa na Katiba.
VOX POP – RULING