Mbunge wa Mwea Mary Maingi ametoa wito kwa Mamlaka ya Barabara Kuu KeNHA kutekeleza haraka hatua za usalama kwenye Barabara Kuu ya Mwea-Embu kufuatia vifo vya watu 10 katika ajali ya barabarani huko Murubara Jumamosi iliyopita. Maingi anataka KeNHA iweke alama za barabarani zinazofaa, kukarabati sehemu iliyoathiriwa na kujenga matuta ya mwendo kasi ili kusaidia kupunguza idadi inayoongezeka ya ajali.
MARY MAINGI – KeNHA